Friday , 11th Jul , 2014

Dashosti ambaye hivi sasa ameachana na muziki wa dunia na kujikita katika muziki wa injili nchini Kenya Size 8 amejiandaa kufanya colabo na msanii mahiri wa nyimbo hizo anayeitwa Willy Paul.

Msanii wa miondoko ya injili Kenya Size 8

Size 8 anayefanya poa na wimbo wake 'Mateke' iliyotwaa tuzo ya video bora ya mwaka kupitia tuzo za Grooves ameelezea kuwa atamshirikisha mkali huyo katika single yake mpya iliyobatizwa jina Tam Tam.

Size 8 ameelezea kuwa wimbo huo unahusu zaidi maswala ya mahusiano na ndoa na hii itakuwa ni colabo yake ya kwanza kwa mwanadada huyo baada ya kuingia katika miondoko hiyo maarufu kama gospel music.