Thursday , 20th Aug , 2015

Baada ya kuingia katika muziki wa injili nyota wa muziki wa kike nchini Kenya Size 8, amezidi kuonesha mashabiki kuwa lugha ya Kiswahili haimpi taabu na kuweza kutumia lugha hiyo katika video ya wimbo wake mpya alioubatiza jina 'Afadhali Yesu'.

nyota wa muziki wa injili wa nchini Kenya Size 8

Size 8 ambaye amekuwa ni shabiki wa magwiji wa muziki wa injili wa kike nchini Tanzania wakiwemo Rose Mhando, Christina Shusho na wengineo wengi Afrika Mashariki, amependezwa kutumia lugha hiyo ya Kiswahili katika wimbo huu mpya.

Mwanadada huyo amekuwa akiweka headline mbalimbali kupitia mitandao ya jamii haswa baada ya kuachana na muziki wa dunia na kuamua kulitangaza neno la Mungu kupitia sanaa yake ya muziki nchini humo.