Monday , 16th May , 2016

Msanii wa Bongo fleva Nuhu Mziwanda ameibuka na kusema kuwa hawezi kurudi tena nyuma hasa katika suala la mapenzi na wala ya nyuma hayajamuumiza yeye anasonga mbele tu.

Msanii wa Bongo fleva Nuhu Mziwanda

Licha ya maneno hayo kutoka kwa msanii huyo lakini baada ya kuachana na Shilole amekuwa akimshutumu mara kadhaa ikiwemo kutokuwa mwaminifu katika uhusiano wao na juzi kati alifunguka kuhusu kumfumania na Madee, madaia ambayo Madee aliyakanusha.

Kuna stori ziliibuka pia kuwa wawili hao walianza kutupiana madongo kupitia nyimbop zao walizoachia baada ya kuachana zikiwemo SAY MY NAME ya Shilole Ft Barnaba na ile ya Nuhu Mziwanda inaitwa JIKE SHUPA aliyomshirikisha ALIKIBA.