Wednesday , 19th Nov , 2014

Baada ya kuachia 'Siri' kazi kali kabisa ya pamoja kutoka kwa Barnaba Classic pamoja na Vanessa Mdee, mastaa hawa wamesema kuwa, mchakato wa video ya kazi hii umepangwa kufanyika huko Afrika Kusini hivi karibuni.

wasanii wa miondoko ya bongofleva Vanessa Mdee na Barnaba

Ikiwa ni moja ya kazi ambayo imepata kuzungumzwa sana mtandaoni kutokana na ubora na utata wa kava lake, Barnaba ameahidi video ya aina yake kwa wapenzi wa muziki.

Kwa upande wa Vanessa, staa huyu amesema imekuwa ni uzoefu wa aina yake kufanya kazi na Barnaba ambaye amekuwa pia msaada mkubwa katika kumrekebisha hapa na pale ili kukamilisha kazi hiyo katika kiwango kinachotakiwa.