
Black Rhino ameyasema hayo leo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha PlanetBongo, na kusema kuwa hajawahi kuwa na ndoto ya kuwa mwanasiasa, isipokuwa iwapo wananchi wakimuhitaji kwenda kuwawakilisha, hatosita kuitikia wito huo.
“Sijawahi kuwaza kuja kuwa mwanasiasa hata siku moja, kabisa, ila ninachoweza kusema ni kwamba iwapo kama itatokea wananchi watanihitaji, wataona nafaa na kwamba naweza nikaenda sehemu nikawawakilisha nikawapigania bungeni, lakini pale ambapo muda wangu utakapokuwa umefika labda, nafsi yangu imeamua kuridhia kwamba ok ngoja nisikilize nguvu hii ya umma, ambayo imeamini kuhusu mimi kwenye hili labda naweza nikajaribu kuingia kwenye siasa”, alisema Black Rhino.
Black Rhino ambaye bado anaendelea na harakati za muziki amesema kuwa yeye kazi ye kubwa ni kuburudisha watu, na ataendelea kufanya hivyo