Saturday , 8th Mar , 2014

Katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani, leo hii ikiwa na kauli mbiu Inspiring Change ….. mbali na shughuli mbalimbali ambazo zimefanyika kitaifa na kimataifa, mastaa mbalimbali hapa nchini nao wamekuwa na

Enewz imepata kuongea na msanii wa muziki Mwasiti Almasi, na vilevile mwanadada Mrembo na Mwanaharakati wa maswala yawahusuyo wanawake, Bi Nancy Sumari ambao wamekuwa na ujumbe huu muhimu kwa wanawake katika siku hii kubwa kwao.

Mwasiti kwa upande wake amesisitiza kuwa wanawake wanatakiwa kupendana na kujiamini kuwa wanaweza kusimama wenyewe na kufanya kitu cha maana bila kusukumwa na mtu, wakati kwa upande wa Nancy ujumbe wake umelenga kuikumbusha jamii juu ya usawa bila kujali tofauti za kijinsia.