Monday , 28th Sep , 2015

Mkuu wa Matukio kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Kwerugira Maregesi amesema kuwa, changamoto mbalimbali za kimaadili katika sanaa hususan muziki kwa sasa ni kutokana na wasanii wengi kutokwenda shule licha ya kuwepo shule nyingi za sanaa.

Mkuu wa Matukio kutoka Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA), Kwerugira Maregesi

Bw. Maregesi amesema kuwa, BASATA imekuwa ikitoa wito kwa wasanii hawa kwenda shule bila mafanikio, akieleza kuwa sanaa sio eneo la kukimbilia kwa kuangalia wasanii waliofanikiwa, na hivyo kujaza wasanii wasiojua miiko ya sanaa.