Friday , 17th Oct , 2014

Msanii wa muziki Shilole ambaye siku ya leo anazindua rasmi video yake mpya ya Kamchukue, ameweka wazi kuwa, mpaka kufikia mafanikio aliyokuwa nayo sasa kisanaa, ilikuwa ngumu sana kutokana na familia na pia mazingira aliyokulia.

Shilole na Anna Peter

Shilole amesema kuwa, tangu alipokuwa mdogo amekuwa akionesha uwezo wa kipekee kisanaa, na dada yake ndiye aliyekuwa anafahamu zaidi hili ila hakuwa na uwezo wa kumsaidia, na hapa anaeleza.