Wednesday , 5th Aug , 2015

Nyota wa muziki na maigizo, Shilole amejikuta akilazimika kuweka bayana baadhi ya taarifa zake za matumizi yake kufuatia hatua ya Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) kufikia uamuzi wa kumfungia kufanya shughuli zake sanaa.

Nyota wa muziki na maigizo Shilole aka shishi Baby

Kwa maneno yake mwenyewe, Shilole ameeleza kuwa matumizi yake kwa siku ni shilingi laki 1, pesa hizi kwa hesabu za haraka zinamaanisha kuwa Shilole kwa matumizi binafsi ya siku hadi siku jumla kwa mwezi anatumia shilingi milioni 3, pesa ambazo kwa mwaka zinafikia jumla ya shilingi milioni 36.

Pia akiwa anaishi katika nyumba anayolipia shilingi milioni 7 kwa mwaka na gharama nyingine za mamilioni ya shilingi yanayomtoka kila mwaka ikiwepo ada za wanawe wawili shilingi milioni 10, jumla ya matumizi haya kwa mwaka yanazidi milioni 53.