Monday , 3rd Aug , 2015

Msanii anayefanya vizuri katika chati za muziki Afrika, Shetta amemtambulisha rasmi mtayarishaji muziki kutoka Commoro, Djobanjo kwa mashabiki wake Afrika Mashariki, akiwa amemleta Tanzania kwa projekti yake nyingine kubwa kabisa.

staa wa muziki Shetta akiwa na mtayarishaji kutoka Commoro, Djobanjo

Shetta ambaye ni moja ya majaji wa mashindano ya makubwa ya kudansi ya Dance100%, amesema kuwa, ameamua kumleta producer huyo hapa nchini kwa kazi kubwa kabisa itakayofuata Shikorobo.

Tazama eNewz kesho kusikia story mbili tatu ambazo tumepiga na Djobanjo, akiwa pia ameeleza mengi juu ya tathmini ya muziki wa Bongoflava.