
Shetta
Shetta ameyasema hayo katika 'Friday Night Live' (FNL) ya EATV wakati akichangia mjadala wa kitendo cha Fid Q kuingia na gari lake ndani ya ofisi za EATV baada ya maneno ya muda mrefu kuwa hana usafiri wake binafsi kusambaa.
"Hii gari kuliingiza ndani ilikuwa ni maalum kwa bwana Fareed kwaajili ya kulionesha au?, mbona mimi gari langu la milioni 150 halijaingia ndani?," aliuliza Shetta alipokuwa akijibu kuhusiana na ubora wa gari lake aina ya Land Rover Discovery na gari la Fid Q aina ya Jeep.
"Gari langu mimi hata Fid Q mwenyewe anajua, ningeamua hela niliyowekeza kwenye gari nikaanzisha kiwanda, basi ningekuwa na mimi namiliki kiwanda cha pampers kingeitwa 'Kaila Pampers'," ameongeza Shetta.
Shetta anatamba na wimbo wa 'Hatufanani' aliowashirikisha Jux pamoja na Mr Blue ambapo unafanya vizuri pia katika mitandao ikiwemo Youtube