Saturday , 17th Jan , 2015

Mtayarishaji muziki kutoka Burn Records, Sheddy Clever amesema kuwa amejipanga kwa mwaka huu wa 2015 kutoka na ladha mpya za muziki ambazo zitakomesha kunakili ladha za nje ya bongo.

Sheddy Clever

Amesema anataka watayarishaji na wanamuziki waache kunakili vionjo vya muziki kutoka Afrika Magharibi, huku akitoa wito kwa watayarishaji kushirikiana ili kusogeza Bongo Flava mbele zaidi.

Sheddy katika mahojiano yake na eNewz amesema kuwa, amekwishakamilisha ngoma kali kabisa na mastaa wanaofanya vizuri, ndani yake zikiwa na ladha mpya kutoka hapa hapa nyumbani, huku akijitapa kufanya muziki ambao huwatengenezea njia hata watayarishaji wengine.

Sheddy amesema kuwa, kwa nafasi ambayo muziki wa Bongo Flava umefikia sasa, tayari umetoboa ukihitaji nguvu ya pamoja ili kuendeleza moto wake nje ya mipaka ya nchi.