Sunday , 1st Jun , 2014

Kundi maarufu la muziki la Sauti Sol nchini Kenya linatarajia kutumbuiza katika tamasha la utoaji tuzo za muziki za Africa Music Awards litakalofanyika jijini Durban nchini Afrika Kusini tarehe 7 ya mwezi huu wa Juni.

Sauti Sol wakiperform kwenye jukwaa la muziki

Mmoja wa wasanii wa kundi hilo linalofanya vyema na video mpya iliyobatizwa jina 'Nishike' aitwaye Bien, ameelezea kuwa wamejiandaa vyema kuwapa mashabiki burudani ya nguvu ambapo pia wataungana pamoja stejini kupaform na kundi nyota la nchini humo Mafikizolo.

Kwa kifupi tu kundi hilo la Mafikizolo linawania tuzo katika kipengele cha kundi bora la mwaka.