Wednesday , 25th Jun , 2014

Kundi la muziki kutoka Kenya, Sauti Sol wameingia kwa kishindo katika ulimwengu wa mitindo ya mavazi na kuonesha uwezo mkubwa, na hii ni kutoka katika ushiriki wao katika kipengele cha mitindo ya wanaume cha jarida maarufu nchini Kenya.

Wanamuziki wa kundi la Sauti Sol nchini Kenya

Katika jarida hili, kutoka Sauti Sol, Bien-Aimé Baraza, Polycarp Otieno, Willis Austin Chimano pamoja na Delvin Mudigi wamejaribu kuonesha ladha na mitoko yao ya kipekee katika mitindo, na kuwaachia mashabiki nafasi ya kuamua ni nani ametokelezea zaidi ya mwenzake.

Wasanii hawa wamekuwa na vipaji vya aina yake katika sanaa ya muziki, na hata mionekano yao kila siku imekuwa ikionyesha umakini mkubwa kimitindo kwa uchaguzi wa mavazi ambayo wamekuwa wakivaa.