Tuesday , 12th Jul , 2016

Lina amesema kwamba wimbo mpya anaotaka kuutoa huo utaitwa samaki na ni wimbo ambao ameamua kufanya remix ya wimbo wa Galaton

LINAH

Baada ya mengi kuzungumzwa na zilizo chini ni kuwa Linah na Billnass ni wapenzi wa siri na hawataki kuweka wazi mahusiano yao ila kwa sasa mambo yanaweza yakawa wazi kwakua mwanadada Linah ametumegea siri kuwa anakuja na wimbo wake wa samaki.

Linah amesema kwamba wimbo huo utaitwa samaki na ni wimbo ambao ameamua kufanya remix ya wimbo wa Galaton Samaki akiwa amemshirikisha Billnass hivyo mashabiki zake wakae tayari kuupokea.

Hata hivyo Linah hakutaka kuweka wazi suala la mahusiano yake na Billnass kwani aliendelea kusema yeye na Billnass ni washikaji tu na ameamua kumshirikisha kwa kuwa ameona voko zake ndio zitaingia vizuri katika wimbo wake huo.