
Dully Sykes
Akizungumza kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Dully Sykes ametolea maelezo juu ya sababu iliyofanya wimbo huo ukawekwa kwenye 'account' ya Harmonize ya YouTube, na siyo kwenye 'account' yake, na kusema yalikuwa ni makubaliano ya kibiashar baina yao.
"Hayo ni makubaliano yetu ya kibiashara wenyewe tumefanya, muziki biashara siku hizi bro, kwa hiyo yale ni makubaliano yetu, tumegawana hivi na hivi, kwa sababu wale ni wadogo zangu pia wamefanya kazi kubwa kuhakikisha kaka yao narudi kwenye nafasi kubwa", alisema Dully Sykes.
Dully Sykes aliendelea kusema kuwa licha ya makubaliano ya kibishara pia ni moja ya kuonesha jinsi gani amewathamini WCB kwa kazi kubwa waliyoifanya kwenye kazi yake hiyo, na upendo alionao kwa Harmonize.
"Mimi nimeweza kuweka kwenye 'account' ya Harmonize kwa sababu ya makubaliano yetu tu, jinsi mtoto alivyokuwa na upendo na mimi, alivyojishughulisha, kwa hiyo mimi mwenyewe na heshima yao ni kubwa sana WCB kwangu, sina budi kuwa nao rafiki namna hiyo tufanye nao biashara kubwa za hivyo kwa sababu ni watu wangu wa karibu sana", alisema Dully Sykes.