Tuesday , 14th Feb , 2017

Msanii wa bongo fleva Rummy ambaye sasa ametoa wimbo uitwao 'Mwari' akiwa na Linah amefunguka na kusema watu wamekuwa wakimuhusisha na biashara ya dawa za kulevya kutokana na muonekano wake.

Msanii wa bongo fleva Rummy

Rummy aliyasema hayo kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio na kusema kutokana na maisha yake na muonekano wake watu wamekuwa wakimuhusisha na kusema ni muuzaji wa dawa za kulevya kitu ambacho anadai yeye hajawahi kufanya. 

Msanii huyo anasema kutokana na skendo hiyo kuwa kubwa alishawahi kuitwa na vyombo vya usalama na kuhojiwa juu ya sakata la uuzaji wa dawa za kulevya lakini anashukuru suala hilo lilikwisha salama na vyombo vya usalama viliona hausiki na mambo hayo. 

"Vijana saizi tunajituma katika vitu tofauti tofauti sasa mtu anapoonekana na mafanikio kidogo inakuja stori tofauti, kwamba huyu jamaa lazima atakuwa anajichanganya huku na huku kwa hiyo anafanya biashara ya unga, mimi sijawahi kujishughulisha na dawa za kulevya, sijawahi kufuatwa kufanya biashara hiyo wala sina marafiki wanaofanya biashara hiyo, watu wanasema nauza unga kutokana na muonekano wangu na life style yangu nayoishi sababu kuna maneno ya namna hiyo kwa jamii yetu inayotuzunguka, mtoto akiwa msafi tatizo, mtoto akiwa anatumia magari mazuri watu wanaona anafanya hayo mambo" alisema Rummy 

Rummy amekiri wazi kuwa tetesi hizo zimekuwa zikumuharibia kwani kuna wakati anashindwa kuwa huru na kufanya mambo yake kwa uhuru kutokana na maneno ya watu, ila anadai katika maisha yake yeye anapenda sana kusafiri, kula vizuri, kuwa sehemu nzuri