
Roma
Roma Mkatoliki anakiri kuwa kwanza kitendo cha kipindi hicho kutenga masaa matatu kwa ajili ya muziki wa nyumbani tu kilileta faraja sana na kuleta hamasa kwa wasanii maana kazi zao zilikuwa zikipata nafasi kubwa zaidi kuchezwa kwenye kipindi hicho.
Mbali na hapo Roma Mkatoliki anakiri kuwa kipindi cha Planet Bongo kimezidi kutoa nafasi kubwa wa wasanii wa rap Tanzania kwa kutenga saa zima kuanzia saa tisa mpka saa kumi kwa ajili ya muziki wa rap pekee.
"Kwa kipindi kirefu sana kumekuwa na malalamiko dhidi ya muziki wa Hip hop na rap kutokupewa nafasi hasa katika Vyombo Vya habari hususani radio na television. Wasanii wa Hip Hop wamekuwa wakilalamika sana kuwa muziki huo haupo sana kwenye 'rotation' hasa za vipindi vya radio. Kilichonisukuma kuandika hivi ni ile faraja ambayo naipata pale ninapoona wadau wa media wanabuni na kutenga Segment ambazo zinakuwa zinaupa nafasi muziki huo" alisema Roma Mkatoli
Roma alizidi kueleza kuwa Planet Bongo imefanya muziki wa hip hop kuwafikia watu wengi zaidi mtaani kutokana na kipidi hicho kutoa nafasi ya muziki huo.
Rapa Roma Mkatoliki (kushoto) akiwa na rapa Moni Centrozone (kulia) walipotembelea studio za East Africa Radio wiki kadhaa zilizopita. Kwenye kipindi cha Planet Bongo.
"East Africa Radio kupitia Planet Bongo mlipotenga ile saa tisa hadi saa 10 mkaiita 'Lisaa Gumu Jeusi' hakika ile ilikuwa ni habari njema sana kwa muziki huo. Na imewafikia wengi na ikawagusa wengi na imewasaidia wengi. Juzi tena kama utani mmeanzisha kitu kinaitwa 'Dakika 10 za Maangamizi' nayo ni 'Platform' njema kabisa kwa jamii ya rap music. Kitendo cha kuifanya bongo fleva ilie peke yake tu kuanzia Jumatatu hadi Ijumaa ni habari njema kwa muziki wa kizazi kipya wa nyumbani. Mbarikiwe sana East Africa Radio" alisisitiza Roma Mkatoliki.
Roma Mkatoliki anasema kutokana na muziki wa rap kupewa nafasi zaidi ndiyo imekuwa chachu na kufanya muziki huo kuzidi kupendwa na watu mtaani, na kufanya muziki huo na wasanii wake kufanya vyema katika matamasha mbalimbali.
"Muziki wa Hip hop / Rap umekuwa ni muziki pendwa sana katika matamasha/Concerts kadha wa kadha zinazofanyika nchini na duniani kote, kwa support hii mnayowapa wana hip hop hadi sasa mnaona wenyewe mapokeo yake yalivyo kwenye Show" alimalizia Roma Mkatoliki