Monday , 7th Jul , 2014

Nyota wa filamu wa Nollywood nchini Nigeria Rita Dominic amekuwa kimya katika tasnia ya burudani nchin humo ambapo mashabiki wengi wamekuwa wakijiuliza kulikoni staa huyo kupotea kwa muda mrefu.

Muigizaji wa Nollywood nchini Nigeria Rita Dominic

Ni hivi karibuni dashosti huyo amekuwa akijiandaa na project zake mbalimbali na aliwashangaza watu alipotuma picha zake akiwa nchini Mauritius aki "party" na nyota mwenzake Majid Michael.

Haikuweza kufahamika zaidi kuhusu ukaribu huo ila Rita ameelezea kuwa alikuwa huko Mauritius kwa mwaliko maalum wa sherehe moja iliyokutanisha mastaa mbalimbali.