Thursday , 23rd Jun , 2016

Mwaandaaji wa muziki wa bongo fleva Rash Don ambaye awali tulikufahamisha kuwa amefanya wimbo na Ray C, ameiambia Enewz kuwa anaomba Ray C asaidiwe kutoka katika kundi la matumizi ya madawa ya kulevya kwani ni kati ya wasanii wanaoiwakilisha nchi.

Rash Don.

Hata hivyo Rash ameiambia Enews kuwa alikuwa tayari kukamilisha baadhi ya nyimbo za Ray C japo walizifanya wakati akiwa katika matatizo lakini amesema alifanya ngoma kali ambazo mwanadada huyo akitoka rehab na akiamua kuziachia hewani zitamuweka pazuri katika bongo fleva.

Rash ameiambia Enew kuhusiana na clip iliyosambaa mitandaoni ikionesha msanii Ray C akichukuliwa na gari la polisi na kusema clip hiyo imemsikitisha sana na kuomba wadau wamsaidie msanii huyo ili kuweza kumrudisha katika hali yake ya kawaida ili aweze kuachia ngoma zake ambazo zipo tayari kwa ajili ya kuachiwa hewani.