Sunday , 8th Nov , 2015

Star wa muziki Q Chilla hivi sasa ameona ni wakati muafaka wa kufanya maandalizi ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake ambaye amedumu naye kwa muda katika mahusiano yao ya kimapenzi.

Staa wa muziki Q Chilla

Q Chilla ameiambia enewz kwamba katika maandalizi yake hayo ya harusi itakayofanyika hapo mwakani, mkali huyo amemwandalia wimbo maalum kwa ajili ya mchumba wake huyo ambaye ni mzaliwa wa hapa nchini Tanzania.

Aidha Q Chilla pia akaelezea kuwa baada ya kutofautiana kauli na msanii mwenzkae TID iliyozaa mtafaruku kati yao kwa muda wa miaka saba hivi sasa, star huyo ameamua kuungana upya na TID kuandaa kolabo yao mpya inayotarajiwa kutoka muda si mrefu.