Tuesday , 9th Sep , 2014

Msanii wa muziki wa Bongofleva Abubakari Katwila almaarufu kama Q Chief amevunja ukimya kwa kupata dili la mkataba wa mamilioni na kampuni ambayo itakuwa ikisimamia kazi zake za muziki zitakazotengenezwa kwa ubora wa hali ya juu.

msanii wa muziki wa bongofleva nchini Q Chief akiwa na Joseph Mhonda

Akiwa menye furaha, Q Chila mwenyewe ameonekana rasmi katika picha akikabidhiwa mkataba huo kutoka Qs Mhonda Company chini ya mmilikiQs Joseph Mhonda ambaye amesema kuwa atasaidia kumrudisha Q Chief katika chati na kumvusha kuelekea mbali zaidi.

Aidha Mhonda ameongea na eNewz na kusema kuwa katika mkataba huo mkubwa na Q Chief watazindua bendi itakayokuwa ikifanya kazi zake na wasanii wenzake watakaosimamiiwa na kampuni hiyo ya Qs Mhonda.

Q Chief amesema kuwa kwa takriban miaka mitano amekuwa kimya katika vyombo vya habari na anga ya muziki ikiwa ni sehemu ya kuyapitia maisha mengine nje ya muziki, ila anamshukuru Mungu kwa kupata mkataba huo mkubwa wa kumrudisha tena kwa nguvu zote kwa mashabiki wake.