Q chief amesema kuwa, anasaidia bendi yake hiyo kwa kuwakutanisha na wasanii na wadau mbalimbali kuwapa semina wasanii ambao atakuwa akifanya nao kazi katika bendi hiyo ambayo itazinduliwa rasmi kwa tukio kubwa la onyesho la burudani jumapili hii.
Akizungumzia uzoefu wake, Q Chief amesema kuwa kuishi na wanamuziki kunahitaji moyo, akiwa sasa amekwishaweka mambo yake sawa tayari kwa kuendesha shughuli zake na bendo hiyo, jukumu ambalo atalifanya sambamba na safari yake kama "Solo Artist'.