
Wakati hapa nyumbani tukishuhudia wasanii mbali mbali wakiwapigia kampeni baadhi ya wagombea urais mwaka huu, huko Marekani pia hali imekuwa kama hii ambapo leo msanii Pharrell Williams ameamua kutangaza kuwa anamsapoti Bi. Hilary Clinton kwenye kinyang'anyiro cha urais kinachoendelea nchini Marekani kwa sasa.
“Ni muda wa mwanamke kuwa pale, wanawake wanafikiria vitu kwa umakini na kwa uchambuzi zaidi na sio kibinafsi, nasema nafurahi kuwa mwanaume lakini nawapenda wanawake, kwamba kama tuna mtu wa kuangalia nchi yetu , anyefikiria vitu kwa ujumla, alisema Pharel.
Pharrel Williams ambaye alikuwa kwenye kipiindi hicho cha televisheni na kutumbuiza wimbo wake wa freedom, amesisitiza akisema kwamba si kama hampendi rais wa sasa, isipokuwa ni zamu ya Bi. Hilary Clinton.
“Si kama simpendi rais wetu wa sasa, najisikia kama ni zamu ya Hillary, watu wako kama wanahitaji rais ambaye tutacheza naye, lakini huyo siye atakaye tatua matatizo yako, unahitaji mtu atakee yachukulia kwa uzito” alisema Pharrel.