Saturday , 22nd Mar , 2014

Mastaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nigeria tayari wametia timu kutoka sehemu mbalimbali, kwaajili ya kushiriki harusi ya msanii Paul Okoye kutoka P Square na ubavu wake Bi Anitha Isama, tukio linalochukua nafasi leo huko Port Harcourt, Nigeria.

Kati ya watu wenye majina makubwa walioonekana wakijivuta kuelekea katika harusi hii, huku wengine wakitua kutoka nje ya nchi, ni pamoja na mwanamuziki Kcee, mchekeshaji Julius Agwu na mwigizaji Susan Peters.

Harusi hiyo inatarajiwa kuacha rekodi ya kipekee kutokana na uwezo mkubwa wa wasanii hawa, umaarufu pamoja na siku nyingi za kujipanga kwa ajili ya tukio hili la kipekee.