Sunday , 16th Aug , 2015

Bata la aina yake sambamba na burudani ya muziki na maonyesho ya Live, yameipamba siku ya jana katika Party in The Park, mitindo, hadhi na furaha ya kiwango cha juu ikitawala nyuso za umati mkubwa uliohudhuria tukio The Green Oysterbay.

Baadhi ya mashabiki waliohudhuria onyesho la Party in The Park

Kivutio kikubwa ikiwa kama ni burudani ya nyongeza ni onyesho la mrembo Feza Kessy ambaye kati ya burudani nyingine, akiwa sambamba na madansa wake aliweza kutumbuiza rekodi yake mpya ya Sanuka.

Kutoka nje ya mipaka ya Bongo, Beatenberg vilevile Black Motion ni kati ya makundi yaliyotia nakshi burudani hiyo kwa midundo na shoo tofauti ya muziki.

Wakali pia waliokinukisha na kusababisha watu wasiweze kutulia katika nafasi zao ni Bendi ya Sauti Sol jukwani ambao shoo yao ilikuwa kama hivi.

Ali Kiba aliweza kuwachekecha watu na kusababisha furaha na shangwe katika eneo la tukio kufikia kiwango cha juu kabisa.

Onyesho hilo la nguvu lilimalizwa na kundi la Mafikizolo ambalo sambamba na Bendi nzima na madansa wake walifanya jukwaa kuonekana halitoshi, vilevile mashabiki kukata kabisa kiu yao ya burudani.

Endelea kutazama EATV ambapo tutaendelea kukujulisha yaliyotokea katika onyesho hilo, tukiwa moja ya wadhamini wa nguvu kabisa wa burudani hiyo ya kukata na shoka.

Fezza Kessy Jukwaani
Ali Kiba Jukwaani
Sauti Sol Jukwaani
Mafikizolo