Wednesday , 20th May , 2015

Star wa muziki Pallaso wa nchini Uganda ambaye pia ni mdogo wa star wa muziki Jose Chameleone, ametangaza rasmi kutoka nje ya Menejimenti ya Team No Sleep aliyokuwa akifanya nayo kazi.

wasanii wa Uganda Jose Chameleone na Pallaso

Pallaso amesema kuwa, kwa sasa hayupo sawa sawa kuzungumzia sababu hizo, akiwataka mashabiki kufahamu kuwa kwa sasa chama lake jipya ni Team Good Music, ama Bullet Proof Soldiers.

Mpaka sasa tetesi mitaani zinahusisha kifo cha ndugu wa msanii huyo AK47, na sababu za yeye kuachana na Team No Sleep kutokana na Chameleone kuweka wazi kuwa, alikuwa akifanya kila jitihada kumuondoa marehemu AK47 katika chama hilo kuelekea siku za mwisho za uhai wake.