Tuesday , 18th Nov , 2014

Msanii wa muziki Pius Mayanja maarufu kama Pallaso pamoja na Meneja wake Jeff Kiwanuka ambao wapo uraiani kwa dhamana wakikabiliwa na kosa la kuvamia na kushambulia mtu, watafikishwa tena mahakamani Jumatatu Novemba 24 kusikiliza kesi yao hii.

msanii Pius Mayanja aka Pallaso wa nchini Uganda

Pallaso ambaye alisababisha fujo hizi katika nyumba ya ndugu yake Weasel TV, amekwishaomba msamaha kwa ndugu yake huyu akiwa sasa anabanwa na mikono ya sheria kwa kutenda kosa hili.

Milioni 8 za Uganda ndiyo kiwango cha dhamana inayomuweka nje msanii huyu, huku dalili zikuonyesha kuwa huenda akapatikana na hatika kutokana na kosa hili alilolitenda akishirikiana na meneja wake na rafiki zake wengine wawili.