Monday , 24th Aug , 2015

Rapa Octopizzo ametumia wakati wake kuzungumza na watoto wa wafanyakazi wa Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) kwa upande wa Kenya juu ya umuhimu wa kusaidia na kuwaonyesha uhalisia wa maisha ya wakimbizi kwa ili kujenga ufahamu wao.

Rapa Octopizzo akiwa na vijana wakati alipotembelea Shirika la Wakimbizi Duniani (UNHCR) nchini Kenya

Rapa huyo ambaye ameachia albam mpya inayokwenda kwa jina Long Distance Paper Chasers, ametumia nafasi hiyo kama balozi wa shirika hilo, ambapo mbali na kutoa somo kwa watoto hao, aliweza pia kuwashirikisha wanae Tracy na Zara katika uzoefu huo.

Hii inakuwa ni sehemu nyingine ya mchango wa rapa huyo kama balozi wa shirika la UNHCR, kuhakikisha anaongeza uelewa kwa jamii kuhusiana na madhara ya ukimbizi, na vilevile kuwatengenezea wale walioingia katika wimbi hilo fursa za kujiendeleza kimaisha.