Wednesday , 25th Feb , 2015

Rapa Nonini kutoka nchini Kenya anatarajia kuonesha uwezo katika upande wa tasnia ya uigizaji kupitia igizo la muendelezo linalokwenda kwa jina Code +254, ambapo ndani yake pia inamhusisha star wa muziki Chegge Chigunda kutoka Tanzania.

Nonini

Igizo hili linalobeba kisa kuhusu harakati za muziki, limetengenezwa mwaka 2010 wakati wa upigaji picha za video ya kolabo ya Nonini, Chegge na Lady B inayokwenda kwa jina 'Kila Mmoja'.

Hii inakuwa ni nafasi kwa mashabiki wa mastaa hawa kuona uwezo mwingine wa vipaji vyao kisanaa.