Thursday , 12th Jun , 2014

Katika jitihada za kuendelea kutengeneza mazingira mazuri zaidi ya wasanii kufaidika na kazi zao, Rapa Nonini ameweka wazi timu inayohusisha wasanii wenzake, maalum kwa ajili ya kazi ya kufuatilia stahili za malipo yao.

msanii Nonini akiwa studio

Timu hii ambayo inatambulika kwa jina PRISK - “Performers Rights Society of Kenya inahusisha wadau kama Nameless, R Kay, Ian Mbugua na wengineo ambao watafanya kazi ya kufuatilia kwa umakini malipo ya wasanii, huku akiwataka wasanii kusajili kazi zao rasmi ili kutambulika.

Hii ni jitihada ya Nonini katika kuleta mabadiliko chanya katika sanaa nchini Kenya akiwa kama moja ya wanaharakati na wasanii wakongwe katika sanaa hiyo.