
NISHA
Pia ameendelea kusema kwamba futari hiyo haina masharti, hivyo anawaalika watu wote bila kujali dini kuweza kujumuika na yeye katika siku hiyo ya kufuturisha kwani sadaka yake hiyo haana idadi wala kiwango cha watu ambao wanatakiwa kuwakilisha siku hiyo.
Hata hivyo Nisha ameendelea kusema kuwa wanategemea kuwa na viongozi mbalimbali katika kukamilisha futari hiyo akiwe Mama Samia Hassan na wengine, na kusema kuwa watu mbalimbali wajitokeze kusaidia watu wasio jiweza na si kwa mwezi mtukufu pekee bali katika nyakati zote