Wednesday , 29th Jun , 2016

Msanii wa kike kutoka bongo ambaye pia ni rapper, Tammy the Badest, amesema hakutarajia kama mchumba wake ambaye tayari ameshamchumbia rasmi, angefkia hatua hiyo, kwani wengi waliamini ni mchezeaji.

Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Tammy the Badest amesema wakati anaanza mahusiano na mchumba wake huyo ambaye ni raia wa Nigeria, na kusema marafiki zake wengi walimwambia wanaume wa Nigeria huwa ni waongo hawana mapenzi ya kweli, lakini ilikuwa tofauti na walivyodhani.

'Rafiki zangu walikuwa wananiambia wanaigeria ni waongo, lakini ilikuwa tofauti jamaa akajiongeza sana, akaleta barua nyumbani kwetu, tena bila mimi kujua kutoka Nigeria, mpaka baba akasema kweli huyu muoaji, na mpaka sasa hivi ameshanichumbia rasmi", alisema Tammy the Badest.

Tammy aliendelea kusema kuwa licha ya kukamilika kwa hatua za uchumba, lakini sala la ndoa kwao bado sana.

"Suala la ndoa bado sana, sana tena, ila kama ameshanichumbia mi naona ni kama ndoa tayari (huku akicheka....)", alisema Tammy the Badest.