Harmonize ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, na kusema kuwa wimbo huo ulikuwa wake lakini Q Chilla alimuomba ili apate kitu kitakachomfanya arudi vizuri kwenye muziki.
"Dulla, yani hiyo nyimbo ilikuwa mi nishaandika tayari nikafanya vocal, alafu Q Chillah akaniambia mdogo wangu nimepata management ya QS mhonda mdogo wangu, asa natakiwa niangalie narudije mdogo wangu, hebu jaribu kunisaidia, kwa hiyo mi nikaona kwa vile mi sina management nikaona sio kesi braza Dulla ngoja niifanye, nikachora ngoma nikamwambia pita humo, kwa hiyo yeye aliipenda beat akataka nimpe nyimbo kama nyimbo, kwa hiyo kuna vitu fulani Mazuu alijaribu kutofautisha", alisema Harmonize.
Wiki iliyopita msanii Harmonize ameachia video ya wimbo wa Aiyola ambao ameifanyia nchini Afrika Kusini, pamoja na wimbo wake mpya unaoitwa kidonda changu.