Friday , 12th May , 2017

Nikki wa Pili ameibuka na kushangazwa na watu wanaowasifia mabinti wakipata mume na kufunga ndoa kuliko wakifanya vyema kwenye masomo, huku akiongeza taasisi ya ndoa huongoza kwa kutesa wanawake.

Nikki ambaye hivi karibuni amekua akiutumia ukurasa wake wa instagram na kuandika mambo yanayogusa jamii amehoji kwamba 

"Yaani ndoa/kuolewa kuna heshima kuliko kuwa mwanasheria au mwasibu? Msichana akifunga ndoa anapata zawadi, sifa, heshima kutoka kwenye familia, ndugu na jamii kuliko akipata degree"- Nikki wa Pili alihoji.

Aidha Nikki amefunguka na kudai dhana ya kwamba kuolewa ni heshima kumewafanya hata watoto wa kike kushindwa kuendeleza vipaji vyao au kutimiza kwa kuwaza ndoa.

"So wasichana wanakuwa na ndoa ya ndoto kuliko hata ya career...cha kushangaza ni kwamba kihistoria ni kwamba mwanamke ameteseka sana katika taasisi inaitwa ndoa lakini bado ndio ndoto yake kuu iliyojengeka kwenye jamii"- Nikki aliongeza

                                                 Ujumbe wa Nikki Mtandaoni