Friday , 11th Dec , 2015

Msanii Young Dee ametolea ufafanuzi kuhusu post yake aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa instagram, na kusema kuwa amefanya hivyo ili kufikisha ujumbe kwa mashabiki wake ambao wanamfuata kwa mtazamo hasi.

Young Dee ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cgha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa iwapo hapati kitu chenye mtazamo chanya kwake, haina haja ya kubaki kuwa shabiki wake.

“Sioni kama kuna haja ya kuendelea kuweka group kubwa ya watu ambao watakuwa wanakuzunguka kwa namna hiyo, kuwa msanii ambaye nina followers karibia laki nne alafu siwezi kupata kitu chochote positive out of it, hiyo inamaanisha watu wengine wanakufuata sio kwa sababu ya kukupa kitu positive, labda ya kukuongezea vitu negativity kwenye maisha”, alisema Young Dee.

Young Dee aliendelea kwa kusema kuwa hakatai kukososlewa na mashabiki wake, lakini pale wanapoona amekusoea ni vyema kumfuata na kumwambia kwa njia nzuri, na si kutoa maoni yasiyo na msingi kwenye ukurasa wake.

“Negativity haimaanishi hautakosolewa, ni kwamba sisi ni binadamu hamna ambaye amekamilika, mimi nina tatizo nifuate in positive way kunisaidia, atleast hata ungemtafuta private huyo mtu ambaye amekosea hiyo ni positivity”, alisema Young Dee.

Young Dee wiki hii aliweka post ambayo inasema kwa shabiki yeyote ambaye atatoa maoni yake ambayo si mazuri kwake, atalazimika kumblock katika ukurasa wake.