Monday , 10th Nov , 2014

Msanii Ney wa Mitego, ameweka wazi ukubwa wa familia yake kwa sasa baada ya kupata mtoto wa kiume mapema wiki iliyopita, kutokana na mtazamo wa tofauti na sintofahamu kutoka kwa jamii na mashabiki wake kuhusiana na ukubwa wa familia yake kwa sasa.

mtoto wa msanii wa muziki wa bongofleva Ney wa Mitego

Ney amewaweka sawa mashabiki wake kuwa, kwa sasa amekuwa rasmi ni baba wa watoto watatu tu, na si vinginevyo, akifunguka kuwa hii haimaanishi kuwa yupo tayari kuanza maisha rasmi ya kifamilia na mama wa watoto hawa, na hapa anafafanua zaidi juu ya watoto wake hawa, kwa faida ya mashabiki wake.