Nyota wa muziki RnB wa nchini Marekani Ne-Yo
Kati ya mastaa hao kutoka afrika Mashariki ni mwanadada Wangechi kutoka Kenya, Alikiba wa Tanzania na Maurice Kirya kutoka Uganda kati ya wasanii wengine.
Neyo ambaye hivi karibuni alikuwa huko Afrika Kusini katika sherehe za tuzo maarufu, anaongeza msisimko katika tasnia ya burudani kupitia ujio wake huo, akielezwa kutoa tamko kuwa anasikia heshima kurudi katika bara hili na kusherekea pamoja na mastaa wa muziki.
Taarifa za awali zinaweka wazi pia kuwa, Nyota huyo atapata nafasi ya kukutana na wadau katika sherehe maalum itakayofanyika tarehe 19 katika eneo ambalo bado halijawekwa wazi.