Monday , 7th Sep , 2015

Star wa muziki Nazizi kutoka Kenya, ameendelea kujikita katika suala zima la kujiweka fiti kimazoezi, akiunganisha nguvu zake katika harakati hizo kwa kushirikiana kwa karibu na mwana mazoezi na rapa maafurufu kutoka hapa Bongo, Zola D.

Staa wa muziki Nazizi kutoka Kenya akiwa katika mazoezi ya masumbwi

Nazizi ameonekana akijifua si tu kupunguza mwili, bali kujiweka fiti pia kwa upande wa mazoezi ya ndondi, mabadiliko makubwa na muonekano wake mzuri ukizidi kuonesha jitihada nyingi ambazo ameziwekeza katika kupiga tizi.

Kama pia njia ya kuhamasisha kundi kubwa la watu wanaotaka kuondokana na unene, star huyo ameweka picha zake wazi kwa njia ya mtandao.