Friday , 1st May , 2015

Staa wa muziki nchini Uganda Navio ambaye kwa mwaka huu ameanza mchakato wake wa kufanya muziki na wasanii wa Afrika Mashariki ameelezea kumkubali sana msanii Mr Blue aka Byser na kuanza mipango ya kufanya naye ngoma.

wasanii Navio wa Uganda na Mr Blue aka Byser wa Tanzania

Navio ambaye anafanya michakato ya kuanza maandalizi ya kushoot video ya wimbo huo mpya uitwao 'Aiyaya' na mkali Blue, ameongea na Enewz kuhusiana na safari yake hiyo mpya itakayoanza wiki ijayo.