Thursday , 10th Sep , 2015

Msanii na mtayarishaji muziki Nah Reel ameweka wazi kuwa rekodi yao ya 'Game', mbali na kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza mashabiki nje ya nchi, imesababisha pia watu kuendelea kuchimba na kufahamu kazi ambazo zilitangulia kipindi cha nyuma.

Msanii na mtayarishaji muziki Nah Reel na mchumba wake Aika wakiwa katika kava la wimbo 'Game'

Nah Reel ameeleza kuwa, mafanikio hayo ni matokeo ya kazi kubwa iliyowekezwa kwa muda mrefu, kujenga picha kubwa ya Navy Kenzo ambayo sasa imeanza kulipa kwa kuonekana na kukubalika na mashabiki hao nje na ndani ya nchi.