Tuesday , 5th May , 2015

Nafasi ya mwigizaji mahiri mwenye asili ya Kenya, Lupita Nyong'o katika filamu kubwa ya Star Wars imefahamika rasmi ambapo mwanadada huyo atacheza kama Maz Kanata, akiwa anajishughulisha na ujangili katika kasri yake.

muigizaji nyota wa tuzo ya Oscar wa nchini Kenya Lupita Nyong'o

Katika filamu hiyo, muonekano wa staa huyo kama ilivyo kwa washiriki wengine, utabadilishwa kwa teknolojia ya kompyuta, katika projekti hiyo ya mamilioni ya pesa.

Staa huyo wa filamu pia ana kazi nyingine kubwa za filamu ndani ya mwaka huu, huko Afrika Kusini na vilevile Uganda, akiendelea kupeperusha vyema bendera ya nchi yake katika anga za kimataifa.