Akiongea kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, Juma Nature amesema anakerwa sana na nyimbo za sasa hivi, kwani nyingi zinahusu mapenzi.
“Nyimbo nyingi siku hizi mapenzi, inaniudhi mimi, tunga nyimbo watu waruke lakini isiwepo na mambo ya ajabu, tunga nyimbo ukitoa kitu kipya angalia na jamii, muziki sio lele mama lazima ukaze”, alisema Juma Nature.
Pia Juma Nature amewataka watu wafahamu hususan wasanii kuwa iwapo utatunga nyimbo ili kutafuta jina na ujiko, basi waelewe hawataweza kuhimili kwenye game la muziki wa bongo fleva.
“Ukitoa nyimbo nyepesi ujue dakika mbili chali kwa sababu wewe unataka ujiko kwenda Marekani, sasa maujiko hayakufikishi popote”, alisema Juma Nature.





