Friday , 5th Jun , 2015

Msanii mkongwe katika tasnia ya filamu Tanzania, Mzee Chilo ameonyesha kuwa licha ya umri mkubwa alionao, anaendelea na kazi ya sanaa, hivi sasa akiwa katika utayarishaji wa tamthilia kubwa kabisa inayokwenda kwa jina 'Ghafla Siku Moja'.

muigizaji nyota wa filamu nchini Tanzania Mzee Chilo

Kazi hiyo inaendelea kwa sasa kuongeza nguvu kwa upande wa utayarishaji tamthilia hapa nchini ambao bado upo chini kufuatia wasanii wengi kujikita katika filamu ambazo huwagharimu bajeti na muda mdogo kukamilisha.

Mzee Chilo akiwa na msisimko mkubwa zaidi, hapa anaeleza juu ya ujio wa kazi hiyo.