Saturday , 7th Feb , 2015

Star wa muziki Mwasiti Almasi ambaye wiki hii alizima taarifa za kuwa na mahusiano na mtangazaji Sam Misago, amekuwa na wakati mwingine wenye changamoto kuwaweka sawa mashabiki juu ya suala hilo.

Sam Misago na Mwasiti Almasi

Hiyo ni baada ya wawili hawa kukutana uso kwa uso katika show ya FNL jana usiku na kutokea kwa matukio yanayozua maswali mengine juu yao.

Moja ya matukio haya ni kitendo cha Mwasiti kumsurprise Sam kwa zawadi ya Birthday kama ambavyo angefanya mtu mwingine kwa mpenzi wake, kitendo ambacho yeye binafsi amedai kinatokana na urafiki wao mkubwa na si mahusiano ya kimapenzi kwa namna yoyote.

Kuhusu Diamond Platnumz ambaye ndiye aliyeibua tetesi hizi kwa post alizoweka katika ukurasa wa Instagram, Mwasiti amesema kuwa msani huyo amefanya hivyo makusudi kwa kutaka kujua undani wa urafiki wake na Sam Misago kutokana na kuwaona kuwa na ukaribu wa muda mrefu ambao hakuuelewa, na si vinginevyo

Kwa upande wa pili kama ulipitwa, Sam Misago mwenyewe kupitia kipindi cha Friday Night Live anachoendesha hapa EATV, amesema kuwa yeye na Mwasiti ni marafiki wazuri, wakiwa wamedumu na urafiki huo kwa miaka 6 sasa kama sio saba.