Wednesday , 11th Nov , 2015

Msanii toka pande za Temeke Chege Chigunda amesema kitendo cha mwanasiasa kuamua kuingia kwenye tasnia ya muziki ni sawa kwani kama binadamu mwingine, anaweza akawa na kipaji zaidi ya kimoja.

Chege ameyasema hayo kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kueleza kuwa mtu yeyote anaweza akawa mwanasiasa na mwanamuziki, ili mradi tu awe na kipaji cha muziki.

"Mi naona ni suala la kawaida kwa sababu kila binadamu ameumbwa na vipaji zaidi ya kimoja sema vitu vingine vinakuwaga bado vimejificha mpaka ajitokeze ndo tunajua kumbe mtu mwengine ana kipaji kingine, kwa hiyo mtu anaweza akawa mwanasiasa na akawa mwanamuziki kama kipaji hicho anacho", alisema Chege.

Chege aliendelea kusema kuwa watu wamekariri kuwasikia watu kwenye muziki bila kujua upande wao wa pili wa maisha.

"Watu wamekrem tu kwamba mtu anaweza akawa anaimba muziki lakini background yake shule aliyopita vitu alivyovisoma anakuwa havijui kwa sababu amezoea kumsikia redioni kwenye masuala ya muziki tu, lakini kumbe mtu amesoma anajua siasa, the same na mtu anaweza akawa mwanasiasa lakini hajawahi kutoa ngoma, kumbe ana kipaji cha kuimba siku anakuja kufanya ngoma watu wanamshangaa", alisema Chege.

Hivi karibuni kumekuwa na wimbi kubwa la wasanii kuingia kwenye siasa, lakini hakuna mwanasiasa anayejulikana kujiingiza kwenye sanaa ya muziki