Wednesday , 10th May , 2017

Mwanamuziki anayefanya poa sana na ngoma kibao mtaani, Abelnengo Damien amefunguka na kusema kwa sasa ameamua kukaa chini na kutengeneza muonekano 'brand' yake ambayo itaweza kumuuza zaidi kwa wakati huu ambao yupo chini ya uongozi.

Belle amefunguka hayo wakati akipiga story na Planet Bongo ya East Africa radio na kusema kwamba baada ya kujitangaza kwa kupitia nyimbo zilizofanya vizuri hapa nchini na sasa ni wakati wake wa kujitengenezea muonekano ambao itakua inamtofautisha na Belle 9 wa miaka minne nitano iliyopita.

"Katika hii brand nachohitaji niangalie ni kitu gani nilikosa wakati nafanya kazi mwenyewe na wakati huu ambao nipo chini ya uongozi. Kama msanii ni wajibu wako kuamua ni jinsi gani utafanya kazi ikiwa ni pamoja na kujua thamani yangu kama msanii"- Belle 9

Msikilize hapa chini akifunguka,