Tuesday , 11th Mar , 2014

Mwanamuziki aliyerithi mikoba ya baba yake aliyewahi kuwa gwiji wa muziki wa dansi nchini Tanzania TX William Moshi, Hassan Moshi TX Jr. anatarajia kuandaa onyesho maalum la utambulisho wa wanamuziki wapya.

Hassan ameelezea kuwa onyesho hilo maalum linatarajiwa kufanyika kesho Temeke jijini Dar es Salaam ambapo licha ya utambulisho wa wanamuziki hao wapya, pia bendi hiyo itaachia nyimbo mpya za kufungua mwaka huu wa 2014.

Roman Mng'ande aka Romario ambaye pia ni mwanamuziki wa bendi hii naye pia amesisitiza kuwa Msondo Ngoma kwa sasa imejiimarisha zaidi kwa sasa na kudai kwamba wanamuziki watakaotambulishwa wataleta mshtuko kwa jamii kwani litakuwa onesho maalumu kuliko yote ya Msondo Ngoma.