Saturday , 14th Jun , 2014

Msanii wa muziki Kefee Don Momoh kutoka Nigeria, maarufu zaidi kama Kefee ameripotiwa kufariki dunia huko nchini Marekani akiwa katika matibabu, sababu ya kifo chake ikielezwa kuwa ni mapafu yake kushindwa kufanya kazi.

Marehemu Kefee Don Momoh

Taarifa hizi zimethibitishwa na afisa habari wa msanii huyu, akiweka wazi kuwa Marehemu Kefee alipoteza fahamu akiwa katika safari ya masaa 14 angani kuelekea huko Chicago Marekani, na baada ya kufikishwa katika Hospitali alipoteza maisha.

Taarifa rasmi ya kifo cha msanii huyu pia imekanusha uvumi uliokuwa unaenea mtandaoni kuwa matatizo ya kiafya yaliyosababisha kifo cha msanii huyu yamesababishwa na ujauzito aliokuwa nao.