
Wimbo huo anaotarajia kuuchia mwezi Januari unakwenda kwa jina la 'Baba do it for me' na anasema anaamini kila mtu utamgusa maana ujumbe wake ni mzuri sana
" Unaposema 'Baba Do it for me" yaani unamaanisha Mungu akufanyie jambo fulani ambalo pengine wewe unakuwa umeshindwa au unaamua kumtanguliza yeye tu katika mambo yako mwanzo hadi mwisho ukiamini kwamba yeye ndiye mwenye uwezo wa kufanya". Alisema Chris Van Destin
Chris Van Destin ambaye kwa sasa makazi yake ni nchini Norway lakini ni mzaliwa wa nchi wa nchi ya Kidemokrasia ya watu wa Congo na anafanya muziki wake kwa lugha ya kiswahili na kingereza maana anaamini ndo lugha ambazo watu wengi watamuelewa vizuri
Nyimbo ambazo amewahi kuziachia na zikavuma sana, zinajulikana kwa jina la 'matatizo' na nyingine ilijulikana kwa jina la 'Nishike mkono'

